
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga RPC Benedict Michael Wakulyamba
amethibitisha tukio hilo lililotokea Oktoba 12 mwaka huu katika kijiji
cha Kwamwenda Kata ya Mlorwa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambapo mtoto
Kessy Kamuje mwenye miaka 3 amefariki kwa kuungua moto akiwa shambani
na mama yake mzazi.
“Ni kweli tukio limetokea jana ambapo mtoto Kessy
aliungua kwa moto baada ya mama yake kumlaza kwenye kibanda cha nyasi
shambani ambacho kilishika moto aliokuwa ameuwasha kwaajili ya kupikia”,amesema RPC Benedict.
Kamanda ameeleza kuwa mama wa mtoto Kessy alifika shambani kwaajili
ya shughuli za kilimo ambapo alimlaza mtoto kwenye kibanda cha nyasi na
akawasha moto kwaajili ya kupika kisha akaendelea na shughuli za kilimo
ndipo Kibanda kikashika moto na kumuunguza hadi kufa mtoto Kessy.
chanzo: zanzibar24.
Comments