Mitandao ya kijamii inachangia kudumaa kwa akili, uvivu na mmong’onyoko wa maadili.

mitandaoMatumizi mabaya ya utandawazi husababisha wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo  yao  kwa  kudumaa kiakili, huchangia uvivu  pamoja  na kuwepo kwa mmong’onyoko wa maadili kwa wanafunzi.

Hayo yalisemwa na wanafunzi  mbali mbali kutoka katika skuli sita  kutoka  Mjini na Magharibi B wakati walipofanya mdahalo unaohusiana na utandawazi huko katika ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini hapa.


Walisema matumizi mabaya  ya mitandao kwa wanafunzi kwa kuangalia picha zisizokuwa na maadili ni miongoni mwa mambo yanayowasababishia baaadhi ya wanafunzi kujiingiza katika vishawishi vibaya.

Mmoja wa wanafunzi hao Ismail Mohamed Awadh kutoka skuli ya mtopepo alisema baadhi ya wazee huwa ni chanzo cha kupotea maadili kwa wanafunzi kutokana na kununuliwa simu ambazo hazikustahiki kuwa nazo kwa wakiti huo.

“Kundi kubwa la wanafunzi ambalo linaathirika katika masuala ya maadili ni wale wanaotumia mitandao ya kijamii kwa muda mrefu, ila hili linatokana na wanafunzi hao kununuliwa simu hizo na wazazi wao”alisema Awadhi.

Aliongeza kusema kuwa “lakini pia simu hizo baadhi ya wakati huwa ni chanzo cha wanafunzi kupata mimba katikia umri mdogo tena akiwa bado ni mwanafunzi”.

Fatma Abdallah kutoka skuli ya Haile Selasie alisema kuwa matumizi ya simu yasiofuta taratibu nzuri kwa wanafunzi pia kunachangia wanafunzi kuiga tamaduni za nchi zilizoendelea.

Alitoa mfanowa hayo kwa kusema kuwa “Utawakuta wanafunzio wanavaa kama walivyo watu wan je ya Zanzibar, huku wakieka kando taamaduni na silka zao wakichangiwa na matumizi ya mitandao ya kijamii”alisema.

Hata hivyo alisema kuwa suala la uvivu kwa wanafunzi katika masomo yao nalo linachangiwa na matumizi mabaya ya utandawazi, hali ambayo mara nyingi huchangiwa  kwa kuwepo mashine mbali mbali za kufanyia kazi hasa za nyumbani ikiwemo kupikia kufulia na kadhalika .

Wanafunzi hao walisema kuwa pamoja na kwuepo kwa hali hiyo lakini bado matumizi ya mitandao ina faida pindi mtumiaji akiitumia kwa  maslahi ya kujiongezea elimu au kutafuta taarifa za maendeleo.

Nae Mwalimu wa Skuli ya Sekondari Fuoni, Fatma Ali alisema  mada iliowasilishwa ni nzuri ambayo imo katika masomo ya Civics  na  English hatua ambayo inaweza kuwasaidia kutoa mbinu tofauti kwa wanafunzi hao kutokana na uwasilishwaji wa wenzao.

Ali alitoa wito kwa wazee kutoa mashirikiano na walimu katika maendeleo ya wanafunzi pamoja na utaratibu mzima wa ulezi kwa wanafunzi ili waweze kuepukana na vitendo vya udhalilishaji kwa wanafunzi hao.

Nae Msaidizi mratibu wa mfuko wa kusaidia  watoto Mariyam  Jecha Salum alisema lengo la mradi ni kuinua ufahamu na uimarishaji kwa viongozi wa mabaraza ya  skuli  yanahusiana na uhifadhi wa mtoto pamoja na kutoa elimu ya stadi za maisha ,kutumia vipaji na mengineo.

Skuli ambazo zilishiriki katika mdahalo huo ni Skuli ya Haile- Sallassie Mwembeshauri ,Rahaleo kwa wilaya ya mjini na magharibi ni Fuoni, Mtopepo B na Mwanakherekwe kongamano hilo limefadhiliwa na Mfuko wa kusaidia watoto (Global Fund for Children) kushirikiana na Jumuiya ya wanasheria Wanawake Zanzibar ( ZAFELA .)

 chanzo:zanzibar24.

Comments