
ZAECA imesema mtendaji huyo Hassan Hija Maduhushi, alitengeneza
kizuka bandaa, ili alipate shamba la serikali na kuepusha wizara yake,
isilikodishe kama inavyofanya kwa mashamba mengine, ingawa baadae
waliutegua mtengo huo.
Mdhamini wa ZAECA Pemba, Suleiman Ame Juma, alisema Maduhushi ambae
ni mtendaji wa wizara ya Kilimo, alimtafuta bibi mtu mzima, anaefanana
na kuwa ni kizuka, ili shamba hilo atamke kuwa ni lake, na lisikodishwe
na wizara yake.
Alisema baada ya maofisa wake, kufanya mahojiano na kizuka huyo
bandia, alitoa ukweli wote, na kusema Maduhushi alimpa ushauri wa siri,
na wa uongo juu ya shamba hilo.
Kizuka huyo, alichukuliwa masafa ya mbali na eneo lililopo shamnba
hilo Mizingani wilaya ya Mkoani, aliwaeleza watendaji wa ZAECA kuwa,
yeye hafamu lolote kwenye shamba hilo la eka tatu.
“Sisi baada ya kumuhoji huyu mama, alisema kuwa yeye alichukuliwa tu
na mtendaji huyo wa wizara ya Kilimo, lakini hajui lolote linaloendelea,
na wala shamba hilo sio la marehemu mume wake”,alisema.
Katika hatua nyengine, Mdhamini huyo wa ZAECA, alisema mtendaji huyo
wa wizara ya Kilimo, baada ya kumuhoji na kulitayarisha jalada la kesi
yake, ili liende kwa DPP, walizindua kuwa, baba yake alishawahi kumiliki
shamba hilo kisheria.
Alieleza kuwa, ingawa baada ya babayake kufariki na mama yao
kutomkalia kizuka, shamba hilo walikuwa wanaendeleza kulilea, na ndio
maana wakati wa zoezi la ukodishaji alitengeneza kizuka, ili libakie
mikononi mwake.
“Kosa atakalo shitakiwa mtendaji huyu wa wizara ya Kilimo ni kufanya
ushawishi wa kutoa ushauri wa siri, kama sheria no 1 ya mwaka 2012, ya
Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar, kwenye kifungu chake cha
37, kinavyoeleza”,alifafanua.
Hivyo, alisema mtendaji huyo baada ya kumalizika kwa taratibu mbali
mbali za kisheria, anatarajiwa kufikishwa mahakamani, kujibu tuhuma
zinazomkabili, mbele yake.
Wakati huo huo, ZAECA inamshikilia mtu mwengine kwa kosa la kupokea
rushwa ya shilingi 100,000 kutoka kwa mtu aliedaiwa kukodishwa
mikarafuu, kihalali.
Mdhamini wa ZAECA Pemba, Suleimna Ame Juma, alisema baada ya kuarifwa
na mtoa taarifa, waliweka mtego ambapo mtu huyo alinasa, muda mfupi tu
baada ya kupokea kiwango hicho cha fedha, kati ya shilingi 400,000
alizotakiwa kutoa.
“Kuna mchezo mchafu kwenye zoezi la ukodishaji mashamba ya mikarafuu
ya serikali na mengine yanafanywa na watendaji wa serikali, masheha,
watu wa kawaida, lakini tunaomba ushirikiano, ili fedha za serikali
zisiishie mikononi mwa wachache”,alisema.
Wakati huo huo ZAECA Kisiwani Pemba, imefanikiwa kuyaibua na
kuyarejesha serikali na kisha kukodishwa mashamba 30 ya mikarafuu,
yaliodaiwa kufichwa, na kuingizia serikali zaidi ya shilingi milioni 84.
chanzo: zanzibar24.
Comments