Mganga
Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Wonanji Timoth amekanusha taarifa za kufariki
kwa watoto 9 waliokuwa kwenye Incubator kutokana na katizo la umeme hapo
jana hospitali ya Mt. Meru, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli
wowote.
Dkt.
Timoth amesema kwamba watoto waliofariki walikuwa wanne na sio 9 kama
inavyoelezwa kwenye taarifa iliyosambaa mitandaoni, na wamefariki kwa
matatizo mengine lakini sio kukatika kwa umeme.
Dkt.
Timoth ameendelea kwa kueleza kwamba moja ya sababu iliyofanya watoto
hao kufariki ni mama kuchelewa kufika hospitali kujifungua kwa kuwa
alijifungulia nyumbani, pamoja na hatari kubwa wanazopata watoto njiti.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments