Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire jana aliachiwa na Polisi waliokuwa wakimshikilia kwa masaa kadhaa tangu asubuhi.
Akizungumza
baada ya kuachiwa na polisi baada ya kuhojiwa kwa saa saba jana, Meya
wa Jiji la Mwanza, James Bwire, alisema hatua hiyo inatokana
kutuhumiwa kutaka kuhatarisha msafara wa Rais Dk. John Magufuli wakati
akiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
“Nikiwa uwanjani nilifuatwa na askari wawili ambao waliniambia nipo chini ya ulinzi.
“Niliwauliza
tatizo ni nini wao walinijibu wamepewa maelekezo kutoka juu kisha
walinipeleka kituo kidogo cha polisi uwanjani na kuniweka hapo.
“Baada ya rais kuondoka uwanjani nilichukuliwa na askari wengine watatu ambao walinipeleka kituo kikuu,” alisema.
Alisema
askari hao waliomfuata uwanjani walimchukua kwa gari dogo binafsi na
alipofikishwa kituo kikuu cha polisi katika ofisi ya RCO (Mkuu wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa), walimueleza kuwa wamearifiwa kuwa
alikuwa ameandaa kitu kibaya kwenye msafara wa rais kitendo ambacho
alidai kilimsikitisha.
“Walipomaliza
kunichukua maelezo niliendelea kukaa pale nje ya ofisi yao na ndipo
alipokuja RCO na kuniita ofisini kwake ambako alinieleza kwamba shida
iliyopo ni ‘sisi kwa sisi tunasigana’.
Aliniambia: “Nyie kwa nyie mnavutana mnatupa kazi ngumu sisi watendaji, kisha akaniruhusu nidhaminiwe na kutoka”.
Kauli ya Rais Magufuli
Akizungumzia
jana suala la Meya huyo kukamatwa, Rais Magufuli alisema ameyaona mabango
likiwamo lililokuwa limeandika kuwa Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire,
amewekwa ndani na Mkuu wa Mkoa ili asionane na rais.
Rais
Magufuli aliwataka viongozi wa Mwanza kuacha malumbano na kukaa meza
moja kumaliza mambo yao kwa kuwa wanatoka chama kimoja.
Alisisitiza kwamba wakiendelea na tabia hiyo hawatafika popote.
“Mkiendelea
kulumbana mtashindwa kutatua kero za wananchi, haya mabango ya mara kwa
mara yanatokea kwa sababu mnashindwa kutatua matatizo yao.
“Wajane
wanadhulumiwa na masikini hivyo hivyo, tambueni mkishindwa kutatua
mgogoro mapema, utawashinda ukikaa muda mrefu,” alisema.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments