
Akizungumza na Zanzibar24 katika ziara ya ukaguzi wa baa za Magharibi
“A” Katibu wa Mahakama hiyo Saleh Ali Abdallah amesema kuna baa bado
zinapinga maagizo yaliyotolewa na mahakama hasa katika suala la usafi
wa afya katika maeneo ya biashara hizo jambo ambalo litaweza kuhatarisha
afya za wateja.
Hata hivyo amesema kuna baadhi ya baa hizo zipo karibu na makaazi
ya wananchi na nyengine zipo karibu na nyumba za ibada hatua kali
zitachukuliwa kwa watakao epuka sheria zilizowekwa.
Zaidi ya baa Ishirini na 8 zimefanyiwa ukaguzi na Mahakama ya vileo
Zanzibar katika Wilaya ya Magharib “A” na kutoa wito kwa wananchi
kuwacha tabia ya kulalamika pembeni badala yake kupeleka malalamiko
yao sehemu husika ili kupatiwa ufumbuzi.
chanzo: zanzibar24.
Comments