Maafisa wa CRDB waingia mashambani mwa wakulima Pemba.

Katika hali isiyo ya kawaida  Bank ya CRDB  tawi la Pemba  imefunga ofisi zake kwa masaa takribani matatu  na kuwafata wakulima wamboga mboga waliokuwepo mashambani mwao kwa lengo la  kuwapatia huduma za kibank  jambo ambalo limewafanya wakulima hao kuanza kutumia  kwa mara ya kwanza kuweka fedha zao  bank badala ya fedha zao  za kuuzia mazao kuzihifadhi nyumbani.


Wakizungumza mara baada ya kufungua Akaunti wasizozitarajia kwenye bonde la kilimo Mtakata baadhi ya wakulima  wa mbogamboga wamesema  hawakuwa na ubishi walipo waona maafisa wa bank ya CRDB wakiingia kondeni ingawa walipo waona walidhani ni viongozi wa serikali wanakuja kuwakagua hivyo walijawa na furaha walipo ona kumbe ni maafisa wa bank kwani wamepata huduma pasi kupoteza muda wala nauli.

Meneja wa CRDB Ahmed Abuubakar amesema wameamua kwenda  kuwafungulia akaunti wakulima kwenye konde kwa kujali muda wao huku bank ikijipanga kuwakopesha wakulima hao wazalishe  zaidi, mikopo itakayo  kuzingatia taratibu za milazao bila ya kuwa na riba ilikukuza kilimo kisiwani Pemba.

Afisa kilimo kutoka wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi  Ali Said Yusufu amesema kufika kwa bank hio kutoa mashirikiano kutasaidia kuwawezesha wakulima Pemba kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na ukosefu wa fedha.

chanzo: zanzibar24.

Comments