Kivuli
cha aliyekuwa mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa,
Edward Lowassa na mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo
(marehemu) vinadaiwa kuitesa CCM.
Habari
kutoka ndani ya chama hicho katika wilaya za Moshi, Siha na Hai zinadai
kuwa vivuli vya wanasiasa hao ndiyo kiini cha kufutwa kwa uchaguzi wa
mwenyekiti katika wilaya hizo.
Wiki
iliyopita, chama hicho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi,
Humphrey Polepole alisema mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec),
umefuta uchaguzi katika wilaya nne. Mbali ya wilaya hizo tatu za Mkoa wa
Kilimanjaro, nyingine ni Makete ya Iringa.
Alisema
sababu ya kufuta matokeo hayo ni kubainika kwamba wagombea
waliojitokeza hawakuwa na sifa pamoja na kubainika kuwepo na viashiria
hatarishi kwa chama hicho kikongwe nchini.
Kutokana
na uamuzi huo, Polepole alisema wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa
uchaguzi katika ngazi hiyo. Taarifa zilizopatikana jana kutoka Moshi
Mjini zimeeleza kuwa tayari makada kumi na moja walikuwa wameshachukua
fomu.
Taarifa
zilizovuja kutoka ndani ya chama hicho katika wilaya za Hai, Moshi na
Siha, zinadai kuwa mojawapo ya ‘viashiria hatari’ ni uwepo wafuasi wa
Lowassa na Ndesamburo waliojitokeza kuwania nafasi hizo.
Wagombea
katika wilaya ya Moshi ni Christopher Lyimo, Alhaji Omar Shamba,
Consolata Lyimo na Elizabeth Minde ambaye ni mwenyekiti aliyemaliza muda
wake na anayetetea nafasi hiyo.
Habari
hizo zimedai kuwa kikundi kimoja cha makada wa CCM, kilichotwaa
majukumu ya maofisa usalama wa chama, kinadaiwa kumwaga sumu kuwa mmoja
wa wagombea alikuwa kwenye payroll ya Ndesamburo.
Hayati
Ndesamburo alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu (2000-2015)
alipoamua kustaafu mwenyewe. Alifariki dunia ghafla mapema mwaka huu.
“Hicho
kikundi kinaoongozwa na kada mmoja (jina linahifadhiwa) kinajifanya
usalama na kusema, (anamtaja mgombea) alikuwa kwenye payroll ya
Ndesamburo ambaye ni marehemu,”
“Hivi
wewe unavyoona ana shida gani mpaka awe analipwa na Ndesamburo wakati
akiwa hai? Ni siasa za kuchafuana na hicho kimetengenezwa na huyo kada
na kundi lake,” alidai kada mwingine wa CCM.
Mbali
na mgombea huyo, lakini mgombea mwingine kati ya hao wanne anatajwa
kuwa “haaminiki”, lakini haikuelezwa sababu za kuwajumuisha wagombea
wote hadi uchaguzi wao kufutwa.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Moshi Mjini, Priscus Tarimo alipoulizwa
kuhusu uamuzi huo wa Nec alisema umekuwa ni changamoto kwao kwa sababu
walishajiandaa kwa uchaguzi.
“Ni
uamuzi wa vikao vya juu kutokana ni taarifa za kiusalama kwa hiyo sisi
hatuna budi kuupokea na leo (jana) wanachama wetu wameanza kuchukua fomu
upya. Tunaenda vizuri,” alisema Tarimo.
Tarimo
alipoulizwa iwapo waliogombea awali na kuonekana baadhi yao hawana sifa
na wana viashiria hatarishi wataruhusiwa kugombea tena, alisema
wanaruhusiwa kwa sababu hawakuzuiwa.
Minde
aliyemaliza muda wake, ambaye ni wakili kwa taaluma alipoulizwa jana
kuhusu hatima yake alisema yuko nje ya Moshi lakini atarejea leo na
atachukua tena fomu kuwania nafasi hiyo.
Mbali
na wilaya ya Moshi, taarifa kutoka wilaya za Hai na Siha zinadai kiini
cha kufutwa kwa uchaguzi wao, ni baadhi ya wanaowania kutajwa kumuunga
mkono Lowassa 2015.
Habari
hizo zimedai kuwa baadhi ya wagombea ambao ndiyo wenye nguvu na
wanaoonekana watashinda uchaguzi huo, wanatajwa kuwa katika mtandao wa
Lowassa wakati akiwania urais ndani ya CCM.
Mara
baada tu ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, alifanya mkutano
wake wa kwanza ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam na
kulalamikia uwepo wa makada wasaliti.
Aidha,
tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015, chama hicho kimekuwa
kikitekeleza mkakati wake wa kujiimarisha na kuwaondoa makada
waliokisaliti katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindani
mkali.
Ushindani
huo ulikuwa baina ya Dk Magufuli na Lowassa ambaye licha ya kuondoka
CCM na kugombea kwa tiketi ya Ukawa, bado alikuwa na kundi kubwa
linalomuunga mkono ndani ya CCM.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments