Ligi kuu Soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2017-2018 unatarajiwa kuanza
rasmi kesho Oktoba 3 kwa kusukumwa michezo minne katika Viwanja vitatu
tofauti.
Kwa upande wa Kanda ya Unguja Mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya
JKU wataanza kutetea taji lao kwa kucheza na Mafunzo mchezo utakachezwa
Saa 8:00 za mchana katika Uwanja wa Amaan, mchezo mwengine utapigwa saa
10:00 za jioni katika uwanja huo huo wa Amaan kati ya KMKM dhidi ya
Jang’ombe Boys.
Na kwa upande wa kanda ya Pemba kesho timu ya Chuo basra wataanza
ligi hiyo kucheza na Hard rock saa 10:00 za jioni katika uwanja wa
Gombani wakati Kizimbani watakuwa na kazi kucheza na Wawi Star saa
10:00 za jioni katika uwanja wa FFU Finya.
chanzo: zanzibar24.
Comments