
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa, amethibitisha kuwepo
kwa Kigaila rumande katika kituo kikuu cha polisi kanda maalum, na
kusema kwamba bado wanamshikilia Kigaila mpaka pale uchunguzi
utakapokamilika na kumpa dhamana, na hatimaye kufikishwa mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Kigaila bado tunaye dhamana yake bado hajapata,
tunaendelea na uchunguzi tukijiridhisha tutampa dhamna na kumpeleka
mahakamani kujibu mashtaka yake”, amesema Mambosasa.
Bw. Kigaila anashiikiliwa kwa tuhuma za kutoa lugha za kichochezi Oktoba 12 katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Chanzo: zanzibar24.
Comments