Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amesema siku za kampuni ya
Ortello Business Cooperation (OBC) inayomilikiwa na Falme za Kiarabu
kuendelea kuwapo katika Pori Tengefu la Loliondo wilayani Ngorongoro
zinahesabika.
Akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Ololosokwani, Dk Kigwangalla alisema mgogoro
wa Loliondo uliodumu kwa zaidi ya miaka 26 sasa utapatiwa suluhu na
Serikali.
“Naomba
wananchi muwe watulivu Serikali yenu inafanyia kazi matatizo ya
Loliondo na kuhusu kampuni ya OBC kama ambavyo nilitaka leseni ya
umiliki wa kitalu hiki ikimalizika mwezi Januari hatutawapa nyingine,”
alisema.
Alisema
kuna sababu nyingi za kutotoa leseni kwa kampuni hiyo ikiwamo kukiukwa
kwa sheria ya vitalu ambayo hairuhusu kutolewa leseni katika eneo lenye
mgogoro na pia ina eneo kubwa la kilomita za mraba 4,500 ambalo
hawalitumii lote kutokana na kuwapo kwa makazi ya watu.
Akizungumza
katika kikao hicho, mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Ololosokwani
ambacho kinapakana na kitalu cha OBC, Koya Timan alisema kampuni hiyo
ambayo inapakana na Hifadhi ya Serengeti imekuwa ikiwazuia wafugaji
kupata malisho na maji.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments