Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeliagiza Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuiondoa Kampuni ya Udalali ya Yono kwenye mradi
wa Dege Eco Village ambayo hivi karibuni ilitangaza kupiga mnada mali
za mradi huo.
Yono
kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilitangaza kupiga mnada
mali hizo ili kufidia deni la kodi ya Sh45 bilioni lililokuwa akidaiwa
mkandarasi wa mradi huo, Kampuni ya Ujenzi ya Mutluhan kutoka nchini
Uturuki.
Mradi
huo ulikuwa gumzo nchini baada ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), kubaini uwapo wa ubadhirifu.
NSSF
waliingia ubia na Kampuni Binafsi ya Azimio Housing Estate Limited,
lakini baadaye ikaibuka shaka ya upotevu wa zaidi ya Sh270 bilioni.
Jana, mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka alitoa agizo hilo baada ya kamati kupitia hesabu za NSSF za mwaka wa fedha 2015/16.
“NSSF
ikanushe tangazo mara moja la kuuza mradi wa Dege ambalo lilitolewa na
Kampuni ya Udalali ya Yono. NSSF iifahamishe TRA kuwa ule mradi si mali
ya mkandarasi, hivyo wawaondoe Yono kwenye eneo la mradi,” alisema
Kaboyoka.
Kamati
pia imeitaka Bodi ya NSSF kuchukua hatua za dharura kwa kushirikiana na
mkandarasi aliye eneo la mradi ili kuokoa mali zilizopo.
“Sasa
ni juu yenu, mtaamua mumrejeshe mkandarasi au mnatumia njia gani ili
mali iliyopo pale isizidi kuharibika na kuharibiwa,” alisema Kaboyoka.
Pia,
aliitaka Bodi ya NSSF kukamilisha mapitio ya mkataba kati yake na mbia
kwa masilahi mapana ya Taifa na taarifa ya utekelezaji ipelekwe kwa
Spika wa Bunge kabla ya Novemba 15.
Awali,
akichangia hoja hiyo, mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
alisema Yono ilitangaza katika mitandao kuwa itapiga mnada mali zilizoko
katika mradi huo ili kufidia kodi anayodaiwa mkandarasi.
Akizungumzia
hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema baada
ya kusikia tangazo hilo waliwasiliana na Yono na walisitisha.
Hata hivyo, wabunge waliwabana viongozi hao wakiwahoji ni kwa nini hawakukanusha tangazo hilo baada ya kubaini halina ukweli.
Makamu
mwenyekiti wa kamati ya PAC, Aeshi Hillal aliitaka NSSF kuhakikisha
mradi huo unafanya kazi hata kama wanataka kuongeza mbia mwingine.
“Hatuwezi kutafuta mbia kwa sasa wakati mradi uko katika hatua hii. Hakuna mtu atakayeweza kukubali.
“Pia,
kuna gharama ambazo zinaendelea kuwapo pale, fanyeni mradi huu hata
kama utaanza kwa awamu kuliko kuendelea hivi na fedha zinaendelea
kutumika na vifaa vinaibwa,” alisema Hillal.
Mwenyekiti
wa Bodi ya NSSF, Profesa Samwel Wangwe alisema wamepokea maagizo hayo
na watakwenda kuyafanyia kazi kama kamati ilivyoshauriwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments