Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imelaani vitendo vilivyofanywa na askari ambavyo havina maadili ya kazi.
Taarifa
ya polisi ya jana Jumanne Oktoba 24,2017 imesema jalada
limeshafunguliwa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini waliohusika
kuwapiga wananchi.
Imeelezwa
askari hao walijichukulia sheria mikononi baada ya mwenzao Charles
Yanga kukutwa ameuawa na mwili wake kuachwa pembezoni mwa uzio wa kambi
ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) iliyoko Ukonga.
Kamanda
wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema Jumapili Oktoba 22,2017
walipokea malalamiko ya watu wanaosadikiwa kuwa askari kufanya msako na
kuwapiga wananchi wanaoishi jirani na kambi ya FFU ambao hawana hatia.
“Jeshi
la Polisi linalaani vitendo hivyo ambavyo havina maadili ya kazi za
polisi. Jalada limefunguliwa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini
watuhumiwa wa tukio hilo. Tunaomba wananchi watoe ushirikiano kutoa
taarifa za wahusika waweze kuwachukulia hatua watu au askari waliohusika
na matukio hayo,” alisema.
Kamanda
Mambosasa amesema Oktoba 21,2017 saa sita usiku maeneo ya kambi hiyo
askari wakiwa kazini walikuta mwili wa askari huyo, huku pikipiki
aliyokuwa akiendesha ikiwaka taa za tahadhari.
Amesema mwili wa askari huyo ulikuwa na majeraha kwenye paji la uso na sikio moja likiwa limekatwa.
Kamanda
Mambosasa amesema walipofuatilia wamebaini askari huyo aliuawa na watu
wasiojulikana na kutelekezwa katika maeneo ya kambi ya polisi.
Amesema kupitia kikosi kazi cha polisi wanaendelea na msako kuhusu tukio hilo la kikatili li kuwabaini watuhumiwa waliohusika.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments