
Katika salamu hizo Dk. Shein alieleza kuwa wananchi wa Zanzibar
wanaungana pamoja na ndugu zao wa Uturuki katika kusherehekea siku hii
adhimu na muhimu katika historia ya nchi hiyo.
Aidha, salamu hizo, zilieleza kuwa tukio hilo kubwa, linatoa nafasi
ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa kati ya Jamhuri ya Watu wa
Uturuki na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo pamoja na familia
yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Uturuki afya na sherehe njema
katika kuadhimisha siku hiyo huku akimtakia kiongozi huyo mafanikio
zaidi katika kuendelea kuipatia maendeleo zaidi ya kiuchumi nchi hiyo
kwa madhumuni ya kulinufaisha Taifa hilo pamoja na watu wake.
Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na Jenerali Kemal Ataturk
ambayo iliundwa na kuwa Taifa baada ya vita vikuu vya Kwanza vya dunia
ambapo kabla ya hapo Waturuki walikuwa chini ya milki ya Osmani (Ottoman
Empare) iliyounganisha mataifa mengi ya Sultan wa Konstantinopoli
wakati huo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk.
chanzo: zanzibar24.
Comments