
Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana pamoja na
ndugu zao wa Zambia katika kusherehekea siku hii muhimu katika historia
ya nchi hiyo ambapo tukio hili la kihistoria lilitokea Oktoba 24 mwaka
1964 ambapo Zambia ilipata uhuru kutoka koloni la Kiengereza.
Aidha, salamu hizo, zilieleza kuwa tukio hilo kubwa, linatoa nafasi
ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa kati ya nchi mbili hizo
hatua ambayo itaimarisha zaidi uhusiano katika nyanja za Kitaifa na
Kimataifa yakiwemo mashirikiano ndani ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Jumuiya
nyenginezo za Maendeleo.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo pamoja na familia
yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Zambia, afya njema na kuwatakia
sherehe njema zenye amani na utulivu wananchi wa nchi hiyo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
chanzo: zanzibar24.
Comments