Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 4 (a) cha Sheria ya
Usajili ya Magazeti na Vijarida Namba 5 ya Mwaka 1988, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein,
amemteua Bwana Yussuf Omar Chunda kuwa MWENYEKITI WA BODI YA USHAURI YA
USAJILI WA MAGAZETI NA VIJARIDA, ZANZIBAR.
Uteuzi huo umeanza tarehe 19 Oktoba, 2017.
Taarifa ya uteuzi huu kutoka Ikulu Zanzibar, imesainiwa na Dkt.
Abdulhamid Y. Mzee, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu
Kiongozi, ZANZIBAR.
chanzo: zanzibar24.
Comments