
Diwani aliyewarekodi viongozi wa Halmashauri ya Meru wanaodaiwa kuwa walikuwa wakiwashawishi kwa ahadi ya fedha na mambo mengine Madiwani wa CHADEMA ili wajiuzulu, amejitokeza na kusema kuwa amewarikodi kwasababu ya maslahi ya taifa na kuchukia rushwa.
Diwani huyo wa Kata ya Mbuguni, Ahimidiwe Rico aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka katika ofisi za Taaisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Arusha ambako alihojiwa kwa takribani saa tatu kuhusu tuhuma hizo za rushwa.
Aidha alieleza kuwa alikutana na maafisa wa TAKUKURU kutoka Makao Makuu Dar es Salaam, ambapo walimhoji na alipoulizwa kuhusu vifaa vilivyotumika kurekodi, alisema kuwa ni mali ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ambavyo alivitoa nchini Uingereza alipokuwa akisoma, na kwamba ushahidi huo walishirikiana kuukusanya.
Mbali na Rico, maafisa hao waliwahoji kwa zaidi ya saa sita, madiwani waliojiuzulu Chadema wanaotuhumiwa na Mbunge Nassari kuwa walipewa rushwa na si kweli kwamba walijiuzulu kwa hiar yao kama ambavyo walidai kwa nyakati tofauti.
Wengine waliohojiwa ni Catherine Mtui, aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu, Japhet Jackson, aliyekuwa Diwani wa Ambuleni na Bryson Isangya, aliyekuwa Diwani wa Maroroni..
chanzo:zanzibar24.
Comments