
Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mohammed Ahmda
Salum amesema licha ya kuwa serikali haina ajira za kutosha lakini
ajira ya bodaboda bado haijaruhusu kufanyika Zanzibar kutokana na
athari nyingi zinazotokea zinazotokana na bodaboda hizo.
Amesema Serikali inawashauri vijana kufanya ajira halali
zilizoruhusiwa kisheria ili kuepusha mizozo na serikali na kutoa
wito kwa waendesha pikipiki kuwa makini na kufuata sheria wanapokuwa
barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu ambayo itamkinga endapo watapata
ajali.
chanzo: zanzibar24.
Comments