
Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Manyara, Longinus Tibishubwamu amesema tukio hilo limetokea mjini
Babati jana saa 12:30 jioni, ambapo bwana Cosmas alikuwa lindoni katika
Benki ya NMB tawi la Babati.
Kamanda Tibishubwamu amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kabla
ya kifo cha mwanamke huyo, kulitokea mzozo kati ya wawili hao kuhusu
fedha za matumizi ya mtoto .
“Wakati wakiendelea na mzozo, ndipo askari huyo kwa
kutumia silaha aliyokuwa nayo alimpiga Regina risasi nne kwenye paji la
uso, kifuani na shingoni,” amesema Kamanda Tibishubwamu na
kuongeza kuwa baada ya tukio hilo mtuhumiwa aliitelekeza silaha lindoni
na kwenda kujisalimisha polisi .
Mtuhumiwa yupo mahabusu kwa mahojiano kabla ya hatua nyingine
kuchukuliwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mji wa
Babati ya Mrara.
chanzo: zanzibar24.
Comments