Askari Magereza watakiwa kutumia rasilimali vizuri.

Mkuu wa Magereza nchini, Kamishna Jenerali Juma Malewa ametoa wito kwa askari wa jeshi hilo kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo ndani ya vituo vyao kutengeneza vijaa vitakavyo tumika kujenga nyumba za makazi ya jeshi hilo kwa bei nafuu

Kamishna Jenerali Malewa ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara huko mkoa wa Pwani kwa lengo la kukagua miundombinu katika gereza la mahabusu la Mkuza,picha ya ndege, gereza la Kigongili wilayani Bagamoyo na kuweka jiwe la msingi katika gereza la Mkuza.


“Pamoja na changamoto nyingi ambazo nimezikuta changamoto kubwa ni makazi ya askari nyumba za askari hazitoshi zilizokuwepo zimechakaa zingine zinahitaji ukarabati mkubwa tu, nimekuja kujionea mwenyewe hali halisi ilivyo ili nikirudi ofisini nione tunafanyaje ili tuweze kusaidia angalau kukarabati ili ziwe katika hali nzuri,lakini kubwa tunalolitaka kwa askari wetu nikutumia rasilimali zilizopo katika vituo vyao vizuri,” alisema Kamishna Jenerali Malewa.

Aidha alikutana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaristi Ndikilo ambapo mbali na kuzungumzia makazi duni ya askari, Mkuu wa mkoa huyo amemuomba Jenerali Malewa kuangalia namna ya kuboresha  maslahi kwa watumishi wake.
chanzo: zanzibar24.

Comments