Aliemtorosha msichana asakwa Pemba.

Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, linamtafuta kijana Mohamed Nassor (25) mkaazi wa Changaweni wilaya ya Mkoani, akituhumiwa kumtorosha msichana (16), aliechini ya uangalizi wa wazazi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Shehan Mohamed Shehan, alisema kijana huyo, alitoroka baada ya kushitukia kuwa anafautwa na Polisi, baada ya kufanya kosa hilo.


Alisema kijana huyo alikwenda kijiji cha Makombeni Oktoba 23, na alipofika, alimtorosha msichana huyo na kumpeleka Changaweni kwa lengo la kumingilia.

Alisema baada ya mtoto huyo kuhojiwa, ndipo taarifa zilipowafikia na kuanza kumtafuta, ingawa taarifa za awali zilionyesha amekimbia.

“Jeshi ka Polisi linamtafuta kila kona, na limeshaweka mitego, ili kuhakikisha anapatikana na kufika mbele ya mkono wa sheria kujieleza”,alisema.

Hata hivyo amewataka wazazi na walezi, kuwa karibu na watoto wao, na kila baada ya muda kujua walipo, ili kuweza kutatua changamoto kama hizo zinapowatokea.
chanzo: zanzibar24.

Comments