
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Lodson, alisema jana kuwa
aliyefariki ni Fikiri Paulo (27), mkazi wa kijiji cha Mlanda wilayani
Chato ambaye mwili wake ulitolewa shimoni akiwa ameshaaga dunia.
Mwili huo ulitolewa shimoni na wachimbaji wadogo, kwa mujibu wa mkurugenzi wa mgodi wa Bingwa, Hussein Nyanzala.
Kamanda Mponjoli alimtaja manusura wa ajali hiyo kuwa ni Musa Evarist (19), mkazi wa kijiji cha Mpomvu.
Alisema Evarist aliokolewa muda mfupi baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mwamba.
Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni kukatika kwa gema la udogo wa
mwamba wa mawe katika shimo walimokuwa wakichimba vijana hao.
Baada ya gema kukatika, imeelezwa, kifusi kuliwafukia wachimbaji hao.
chanzo: zanzibar24.
Comments