
kauli hiyo ameitoa leo mara baada ya Spika wa Bunge la jamhuri ya
muungano tanzania Job Ndugai kuagiza wabunge Zitto Kabwe na Saed
Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge
kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni.
“Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni
heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya
Maadili, Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu
kushuhudia mbunge anapigwa risasi mkutano wa bunge ukiendelea wabunge
wazoefu tulikuwa na matumaini makubwa na spika Ndugai tulimpigania dhidi
ya njama za kumhujumu kutoka Ikulu anatuangusha angejua nguvu aliyonayo
kukabili udikteta unaonyemelea nchi yetu asingehangaika na ukosoaji
wenye staha tunaoufanya” alisema Zitto Kabwe
Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa Ndugai alitamani kufikia japo robo ya
marehemu Sitta katika kuongoza shughuli za bunge lakini ameshindwa
kufikia hata asilimia ya Anna Makinda.
“Kwenye mazishi ya Spika wa watu Mzee Sitta, Ndugai
aliomba afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda
miaka 2 sasa hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa na Rais kwamba
aliuliza wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge” alisema Zitto Kabwe.
chanzo: zanzibar24.
Comments