Zitto akamatwa Uwanja wa Ndege Dar.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT –Wazalendo), Zitto Kabwe amekamatwa na polisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Kigoma.
Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis amesema Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho amekamatwa jioni hii.
Leo Jumatano asubuhi, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema Zitto atafutwe, akamatwe na kufikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Alisema Zitto alipewa barua ya wito wa kufika mbele ya kamati hiyo baada ya Spika Job Ndugai kuagiza hilo lifanyike lakini hajalitekeleza.
chanzo:Mwananchi.

Comments