Waziri Mkuu Ataka Ulinzi Uimarishwe Kwenye Maeneo ya Viwanda na Uwekezaji Dhidi ya " Watu Wasiojulikana ".
WAZIRI
mkuu,Kassim Majaliwa amezitaka serikali za vijiji na ngazi nyingine
mkoani Pwani,kujikita kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo
ya viwanda ili kulinda mali na usalama wa wawekezaji na watanzania
kijumla.
Amesema
haijajulikana hadi sasa nia na dhamira ya watu wasiojulikana
wanaojihusisha kupoteza maisha ya watu ,na ni hatari endapo watajiingiza
katika maeneo ya uwekezaji kwani hakuna mwenye uhakika wa azma yao.
Aidha
Majaliwa ,ametoa wiki mbili kwa waziri wa maji kutathmini matokeo ya
mwenendo wa mradi wa maji wa WAMI ,ili kutoa utaratibu na kama sheria
inaruhusu kuvunja mkataba ikiwa mkandarasi ameshafikia kiwango cha
asimilia 50 ya utekelezaji.
Waziri
huyo ,pia ameziagiza halmashauri nchini kuona umuhimu wa kutenga fedha
kwa ajili ya kununua magari ya zimamoto yatakayosaidia kudhibiti majanga
ya moto yanapotokea hususan kwenye maeneo ya uzalishaji na viwanda.
Katika
hatua nyingine amelitaka shirika la umeme Tanesco,Dawasco kuhakikisha
wanaboresha miundombinu ya umeme na maji katika maeneo yenye uwekezaji
ili kuvutia wawekezaji.
Alitoa
rai hiyo,wakati wa ziara yake ya siku moja ,aliyoifanya mkoani Pwani
kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni cha KEDS kilichopo Kibaha,na
cha kutengeneza vigae Twyford Ceramics Ltd/Pingo,Chalinze ,Bagamoyo.
Majaliwa ,alieleza kuwa ni lazima raia mmoja mmoja na jukumu la kila mmoja kusimamia kulinda nchi kuanzia maeneo wanayoishi .
Alisema
serikali imejipanga kuendelea kusimamia amani na utulivu,ambapo
amewataka wananchi waiunge mkono serikali kupambana na wahalifu wasio na
nia njema na serikali.
“Hatuna
uhakika kwa watu hawa wanaofanya vitendo vya ovyo,watanzan ia waungane
na serikali,kupambana ili wasije kuingia kwa wawekezaji na kupoteza
ndoto za serikali za kupata wawekezaji “alisema Majaliwa.
Akizungumzia tatizo la uhaba wa maji ,alisema mradi wa WAMI ulikuwa ukamilike tangu mwezi July mwaka huu.
Alisema
alitembelea mradi huo mwezi juni mwaka huu ukiwa chini ya asilimia 38
na kusema mkandarasi akiendelea kusuasua watamfukuza na kutoa agizo
ikifika mwezi huu wafikie asimilia 80.
“Nilitaka
kuja mwezi huu lakini nikaambiwa speed ni ndogo na bado hali
hairidhishi,na mkandarasi hajamaliza”mbunge wa Chalinze Ridhiwani
Kikwete amekuwa akiuliza juu ya kukwama kwa mradi huo” ;”Nimetoa wiki
mbili kwa waziri aangalie dhamana ya kampuni kwenye ubalozi wao wa India
na kuangalia sheria namna ya kufanya ama kukamilisha mradi kwa muda
mfupi uliobaki”alifafanua.
Kuhusu
nishati ya umeme Majaliwa,alisema serikali ipo mbioni kutekeleza mradi
mkubwa wa umeme stiegler’s gorge katika chanzo cha mto Rufiji,
utakaozalisha megawatts 2,100 zitakazoondoa kama si kumaliza upungufu wa
umeme uliopo.
Aliitaka halmashauri ya Chalinze,ijipange kwa matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro na kuondoa usumbufu kwa wawekezaji.
Kuhusu
suala la zimamoto ,Majaliwa alisema mkoa huo kwasasa una viwanda
vikubwa hivyo wakati serikali ikipokea changamoto ya uhaba wa vifaa na
magari ya zimamoto ,halmashauri ijipange kupitia bajeti zao.
“Viwanda
hivi ni vikubwa vinajengwa ,kiwanda hiki cha KEDS kina jengo hilo hapo
lenye urefu wa mita 30 juu,tuombe mungu moto usitokee ,unawezaje kuzima
moto kwa maji ya kwenye ndoo ,ipo haja ya kuangalia namna ya kutatua
changamoto hii”
“Dar
es salaam ambako ni mji wa kibiashara serikali itasaidia katika kununua
mitambo ya kusaidia kuzima moto kutegemea ukubwa wa majengo
yaliyopo”aliongeza Majaliwa.
Kwa
upande wa miundombinu ya barabara,alitoa rai kwa halmashauri ya Mji wa
Kibaha kuboresha barabara zilizopita mitaani na kuhakikisha mitaa yote
iwe na barabara bora kwa kufumua zisizofaa na kuchonga barabara zenye
viwango.
Pamoja
na hayo ,Majaliwa alibainisha uwekezaji kama huu unaendana na dhana ya
Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda ambapo itaongeza
pato la nchi na itazalisha ajira kwa wingi.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments