Walia na kichaa cha mbwa hatimae SMZ kutoa chanjo ya mbwa na paka Pangawe aunguja.

Wakaazi wa pangawe walia na wafugaji wa mbwa na paka wanaodhurura ovyo ambao mara nyingi husababisha madhara makubwa kwa wakaazi wa eneo hilo. wametakiwa kuwapeleka wanyama wao kupatiwa chanzo ili kunusuru matatizo yanayoweza kujitokeza katika jamii.

Akithibitisha hilo Sheha wa Shehia ya pangawe Abdallah Juma Mtumweni amesema katika kupambana na zoezi hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kesho wanatarajia kuendesha zoezi la chanjo na kuwaomba wenye wanyama hao kutumia fufsa hiyo.


Serikali kwa makusudi ilikuwajali wananchi wake wameamua kutoa tena chanjo hizi za maradhi dhidi ya kichaa cha mbwa, kwaiyo nawaomba wanajamii nawaomba ten asana wajitokeze kwa wingi kila mwenye mbwa awalete ili kupatiwa chanjo hii kwani chanjo hii inayotolewa ni inaleta manufaa kwetu sote sio watoto tu bali hata watu wazima kwani mbwa kichaa hachagui rika yoyote ya kumg’ata binadamu”

Kwa upande wake mkaazi wa eneo hilo Issa Muhammed Zonga amefahamisha kuwa athari ya kichaa cha mbwa ni kubwa ikiwemo gharama na hata kusababisha kifo.

“ homa ya kichaa cha mbwa ni homa mbaya sana kwasababu unapokosa huduma mapema hatimayake husababisha kifo. Kwakweli nawambia wanaofuga mbwa na hata paka wasidharau kuwapeleka Hospitali kusubiri kwamba mpaka wapate athari ya maradhi na baadae kupita mitaani kuathiri wananchi, Siku wanayosikia kuwa madaktari  wanakuja kwaajili ya wanyama wapeleke wanyama wao kwenda kupiga sindano kwa usalama wa wananchi”.
chanzo: zanzibar24.

Comments