
Tukio hilo lilitokea juzi wakati ofisa huyo alipokwenda kuangalia
utekelezaji wa agizo la siku 14 alilolitoa Agosti 27 kuwataka wakulima
hao wawe wameondoka katika bwawa hilo.
Ofisa huyo alisema alikwenda eneo hilo akiwa amefuatana na baadhi ya
viongozi wa mtaa kukagua iwapo wakulima wameondoka, lakini waliwakuta
wakiendelea na kilimo kwenye vyanzo vya maji.
“Nilipofika eneo hilo
nilikuta wakulima zaidi ya 19 wakiendelea na kilimo, baadhi wakipanda
nyanya na mahindi. Nilianza kuwapiga picha kupata ushahidi, walipobaini
walinishambulia kwa fimbo huku viongozi niliofuatana nao wakitimua
mbio,” alisema ofisa kilimo, Jamila.
Alisema baada ya kuanguka, wakulima walitimua mbio na majembe yao na
fahamu zilipomrudia alienda kituo cha polisi kuchukua fomu kwa ajili ya
matibabu ambayo aliyapata katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga na
aliruhusiwa kurejea nyumbani.
Mtendaji wa Kata ya Igunga, Robert Mwagala amesema Polisi kwa
kushirikiana na raia wema watawasaka wakulima waliomshambulia ofisa
kilimo huyo.
Diwani wa Igunga, Charles Bomani alisema kitendo kilichofanywa na
wakulima hao hakikubaliki, hivyo ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao.
Baadhi ya wakulima waliotii agizo la kuondoka kwenye bwawa hilo
wameliomba Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka juu ya watu
waliofanya ukatili huo.
chanzo: zanzibar24.
Comments