Amesema hayo baada ya Mbunge wa Nzega Mijini (CCM), Hussein Bashe kuomba mwongozo akitaka kamati hiyo ikutane na vyombo vya ulinzi na usalama kujadili jambo hilo.
Bashe amesema kama Spika ataridhia baada ya kupokea ripoti hiyo baadaye pelekwe bungeni ijadiliwe.
Akijibu mwongozo huo, Spika Ndugai amesema kabla ya kufikia Ijumaa wiki ijayo iwe imewaeleza wamefikia wapi.
Bashe amerejea matukio mbalimbali yaliyojitokeza siku zilizopita ikiwemo ya utekaji na Nape(Nnauye) kutishiwa kwa bastola.
Bashe amesema vyombo vya ulinzi na usalama vilitoa taarifa kuwa vinafanyia uchunguzi masuala hayo lakini hadi leo hakuna majibu.
Amesema na jana Lissu(Tundu) alipigwa risasi tena katika nyumba wanazoishi viongozi wakiwemo mawaziri.
Bashe amesema matukio hayo yanaharibu taswira ya nchi duniani hivyo ni vyema kamati hiyo ikakaa na vyombo vya ulinzi na usalama na kupeleka taarifa kwa Spika.
chanzo:Mwananchi.
Comments