
Muungano wa kihafidhina wa Bi Erna
Solberg unawania nafasi ya kurejea madarakani kwa kipindi cha
pili.
Endapo atafanikiwa atakuwa ni mwanamke wa kwanza kutoka chama cha
mrengo wa kulia katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kuchaguliwa
katika nafasi ya waziri mkuu.
Chama cha upinzani cha Labour kinaonekana kutetea nafasi yake ipasavyo kama chama kikuu katika bunge la nchi hiyo.
Kampeni
za uchuzi huo mkuu zimelenga na kuzungumzia vilivyo suala la kodi,
pamoja na kupunguzwa kwa ushuru kwa watunga sera ili kuongeza ukuaji wa
uchumi, wakati chama cha Labour chenyewe kimejikita katika ahadi ya
kuboresha huduma za umma.
Bi Solberg ametawala katika ushirika na chama cha kupambana na wahamiaji .
chanzo:Bbc.
Comments