
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo wa laini amesema kutokana
na matatizo mengi yanayowakumba wazee, serikali kwa makusudi imeamua
kuzindua laini hiyo yenye namba 0774107070 kwa ajili ya kuwasaidia wazee
kuweza kutoa taarifa popote alipo atakapopata matatizo ambayo wazee
watatumia bure bila ya malipo.
Hata hivyo Shadia ametoa wito kwa masheha pamoja na jamii
inayowazunguka kuwa na moyo wa kujitolea katika kuwasaidia wazee ili
kuwaondolea usumbufu.
Kwaupande wa wazee walio hudhuria katika uzinduzi huo wamesema
wamefarajika kuona serikali imeweka mipango na mikakati imara kwa ajili
ya kuwasaidia wazee ikiwemo kuwasaidia huduma za mawasiliano ya bure
kwa ajili ya kutoa taarifa zao.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments