
Akisoma hutuba ya kamati hiyo katika kikao cha Baraza la wawakilishi
chukwani nnje kidogo ya mji wa Zanzibar Mwenyekiti wa kamati hiyo Omar
Seif Abeid amesema licha ya serikali kuwa na utaratibu wa kuwasidia kaya
masikini lakini kaya hizo zimekuwa hazinufaiki na miradi hiyo kutokana
na kushindwa kusimamiwa.
Aidha ametowa wito kwa taasisi zinazosimamia mradi wa kaya masikini
TASAF kufanya kazi kwa bidii ili wananchi waweze kunufaika na maradi huo
katika kujikwamua kiuchumi..
Akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wawakilishi, Waziri wa nchi
ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohamed Aboud Mohamed amesema kutokana
na fedha nyingi kutumika kwa ajili ya kuendeleza miradi hiyo serikali
itaendelea kuzikumbusha taasisi husika ziendelee kuisimamia na
kuiendeleza ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Hata hivyo amesema zaidi ya kaya mia 3 hapa Zanzibar zimepoteza sifa
za kuendelea na TASSAF kutokana na matukio mbali mbali ikwemo wananchi
kuhama makaazi yao na wengine kupoteza maisha.
chanzo:zanzibar24.
Comments