Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na
kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
kutokufika polisi na kutoa maelezo yake.
Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo.
Amesema
upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu
mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya
Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo.
“Wamiliki
wa gari tumewahoji na tunapogundua hakuna muunganiko wowote basi
tunaachana nao maana hakuna haja ya kuendelea kuwashikilia au kushikilia
gari hizo,” amesema.
Hata
hivyo Kamanda Muroto amesema anasikitishwa na kitendo cha aliyekuwa
dereva wa mbunge huyo wakati wa tukio kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi
la polisi.
“Tunasikia
yupo nje ya nchi na hadi leo hajaitikia wito wa kufika polisi kupata
maelezo yake ambayo yangesaidia katika upepelezi wa tukio hilo.”
chanzo:mpekuziblog.
Comments