
Mbunge
wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amesema kitendo cha Tundu Lissu
kusalimika kifo kwenye tukio la kupigwa risasi ni Mungu tu ndiye
aliandika, lakini kinamuumiza zaidi huku akilaumu ameikosea nini nchi
mpaka kufanyiwa hivyo.
Kupigwa
risasi kwa Lissu, ambaye alikuwa Dodoma kutekeleza majukumu yake ya
kibunge, kuliwaibua wabunge walioliomba Bunge kuunda timu ya kwenda
jijini Nairobi kumjulia hali mwenzao, lakini kiti cha spika kilikataa
hoja hiyo kwa maelezo kuwa tayari baadhi yao walishaenda kuwawakilisha.
chanzo:Mpekuziblog.
Wabunge
ambao wakati huo walikuwa Nairobi ni Freeman Mbowe, ambaye ni
mwenyekiti wa Chadema na mbunge wa Hai, na Mchjungaji Peter Msigwa,
ambaye ni mbunge wa Iringa Mjini wa chama hicho.
Wakati
wabunge wakilalamika kukosa ruhusa ya Bunge, kulikuwa na malumbano
kuhusu ushiriki duni wa Serikali na Bunge katika kumuuguza Lissu
aliyepigwa risasi katika kipindi ambacho alishatoa malalamiko kuwa
kulikuwa na watu asiowafahamu waliokuwa wanamfuatilia.
Lakini,
Nyalandu alijitokeza na kwenda Nairobi kumuona Lissu, akiandika katika
akaunti zake za mitandao ya kijamii kuhusu safari hiyo na maendeeleo ya
ziara yake, huku akituma picha zinazomuonyesha akiwa hospitalini.
Mbali
na kumjulia hali na kuhimiza wananchi wamuombee, harakati za Nyalandu
zimekuwa zikiambatana na ujumbe unaonekana kuwa na utata, ambao
umemfanya atafsiriwe tofauti, akihimiza wananchi upendo, amani,
kuvumiliana na haki kushinda dhuluma.
Pia,
Nyalandu, ambaye amekuwa mbunge tangu mwaka 2000, amelielezea tukio la
kushambuliwa kwa Lissu kuwa ni kurudi nyuma kidemokrasia huku akiwaita
waliomshambulia kuwa ni waonevu na kutaka Serikali ifanye jitihada
kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki.
“Sote
tuungane katika kufanya maombi maalumu kwa ajili ya #TunduLissu, na kwa
wale walio karibu na mji wa Mbeya, naomba muungane nami katika Kanisa
la Ebenezer,” ameandika Nyalandu katika ukurasa wake wa Instagram.
Katika video aliyotuma kwenye ukurasa huo, Nyalandu anasema: “Nimekuja
Mbeya kulikumbusha Taifa kuwa kupigwa kwa mmoja wetu ni kupigwa kwetu
sote, kuumizwa kwake ni kuumizwa kwetu sote, na kudhulumiwa kwake huyo
mmoja ni dhuluma dhidi ya kila Mtanzania.
“Tundu
Lissu amepona kwa kuwa imeandikwa (katiba Biblia) ‘hatasinzia yeye
akulindaye’, na kwetu kama Taifa, tukasimama naye wakati huu wa
kujaribiwa kwake. Naamini ndani ya moyo wake akiwa katika maumivu lukuki
aliyonayo, #TunduLissu atakuwa anajiuliza nimekukosea nini Taifa.”
Wakati
katika baadhi ya maeneo, watu walizuiwa kukusanyika kufanya maombi kwa
ajili ya mwanasiasa huyo, Nyalandu anahimiza katika ujumbe wake kuwa
Lissu aombewe “kimya, na tumwombee kwa sauti, tuombe mahali pa
sirini, na tuombe hadharani”, akisema kuwa wameagizwa “kulia na
wanaolia, kwenda kuwaona wagonjwa na waliofungwa, na tuwatangazie
kufunguliwa kwao”.
“Naaam, hii ndiyo siasa sahihi ya utu kabla ya itikadi, upendo kabla ya visasi; heshima kabla ya husuda,” anasema Nyalandu.
“Watanzania
wote tusimame, miguu yetu ikatiwe utayari, roho ya mapenzi na ujasiri
ikatamalaki na kuondoa roho ya hofu na ganzi (spirit of indifference),
tukaipandishe tena bendera yetu pale kileleni Kilimanjaro.
“Yamkini
kwamba haki iishinde dhuluma; umoja wetu, ushinde roho ya matengano; na
sauti za walioteswa na kuonewa zisikike na kuleta tena tumaini jipya la
amani, haki, upendo, na mshikamano.”
chanzo:Mpekuziblog.
Comments