Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendea kuwatunza Wazee waliopo kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikwemo Afya na Makaazi bora.
Akifungua kongamano la kubadilishana Mawazo wazee ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha siku ya wazee duniani,Naibu Waziri wa Uwezeshaji Wazee, Vijana ,Wanawake na Watoto Shadia Muhammed amesema kutokana na umuhimu Mkubwa wa wazee serikali itaendeleza azma yake ya kuwatunza wazee hao ili kuthamini michango walioitowa enzi za ujana wao.
Aidha ametowa kutokana na kukithiri vitendo vya Udhalilishaji katika jamii ni vyema kwa Masheha kutoa taarifa pindipo watapo baini kuna wazee wanafanyiwa vitendo vya udhalilishaji katika jamii ili wawezee hao waweze kutunzwa katika mazingira salama.
Kwa upande wao Wazee na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee Zanzibar JUWAZA wameipongeza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua mbalimbali wanazozichukuwa katika kuwasaidia wazee hao ikiwemo kuwapatia pencheni kila mwezi kwa wazee waliofikia umri wa miaaka 70.
Wesema serikali ya Zanzibar imekuwa mfano mzuri kwa matataifa mbalimbali kujua na kuthamini uwepo wa wazee katika nchi.
Aidha awametowa wito kwa taasisi Binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwasaidia wazee ili wazee hao waweze kunufaika na huduma za maendelea zilizopo hususan katika upatikanaji wa huduma Muhimu ikiwemo matibabu.
Wakati huo huo Mfanya Biashara kampuni ya Bopar enterprises limited Saidi Nassor Bopar ametowa msaadaa wa Sabuni,Nguo na Ndoo kwa wazee hao ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia wazee.
Siku ya wazee inatarajiwa kuadhimishwa ifikapo Octobar mosi ambapo kwa Zanzibar maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika kijiji cha chwaka Wilaya ya kati Unguja.
chanzo:Zanzibar24.
Comments