Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema hakuna haja ya kuanza
kuhangaika kutafuta wachunguzi kutoka nje kwa ajili ya kufuatilia
wahusika wa shambulizi la Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu
Lissu kwa vile vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinajitosheleza na
vina weledi na kazi hiyo.
Waziri
huyo amesema haoni kwa nini baadhi ya watu wanasisitiza kuletwa kwa
wataalamu wa nje kwani hata kama wataletwa bado watalazimika kufanya
kazi kwa mazingira ya Kitanzania wakitumia wataalamu waliopo na hata
ikiwekezana watahukumiwa kwa kutumia sheria za nchini.
“Nchi
yetu inajitegemea hakuna haja ya kuleta vyombo vya nje kufanya
uchunguzi...upelelezi utafanywa na vyombo vyetu, watafikishwa katika
vyombo vya muhumu na watahukumiwa na watoto wetu,” alisema.
Hivi
karibuni Chadema ilitaka wachunguzi nje kuendesha upelelezi kuhusiana
na tukio la kushambuliwa kwa Lissu ikidai kuwa hatua yake hiyo
haimaanishi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havina uwezo bali
vimetuhumiwa katika tukio hilo.
Hata
hivyo, Waziri Nchemba alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama
daima viko macho na vinaendelea na kazi ya kuwasaka wale wote
wanaojihusisha na matukio ya kushambulia watu.
Amesema
suala la uchunguzi haliwezi kukamilika kwa siku moja akitolea mfano
jinsi Marekani ilivyotumia muda mwingi kumsaka mtuhumiwa wa ugaidi,
Osama bin Laden aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaida.
“Uchunguzi
hauna ukomo...unaisha pale tu wanapokamatwa wahusika wote lakini
vinginevyo uchunguzi hauishi maana hata Marekani walimtafuta Osama kwa
muda mrefu sana hawakusema sasa tumesitisha kumsaka,” amesema.
Kiongozi
huyo wa Al Qaida aliuawa Mei 2, 2011 na vikosi vya Marekani
vilivyoendesha operesheni maalumu iliyoratibiwa kutoka Pentagon na
kufuatiliwa kwa karibu na Rais Barack Obama ambaye hivi sasa amestaafu.
Osama alikuwa amejichimbia katika maficho yake nchini Pakistan katika eneo lililojulikana Abbottabad.
Waziri
Nchemba aliwatumia salamu wale wanaojulikana kama ‘watu wasiojulikana’
akisema kasumba ya wahalifu wachache kufanya mauaji na kisha kujinadi
kwa jina la watu wasiojulikana inaelekea ukingoni.
Ameeleza kuwa dakika za wale wanaojihusisha na uhalifu huo kufikishwa kwenye mkono wa sheria zinahesabika
chanzo:Mpekuziblog.
Comments