
Wazazi wa binti huyo, wamesema kuwa mpaka majira ya saa nne usiku
kuamkia Jana Septemba 7 alikuwa nyumbani kabla ya kuwasili kwa vijana
watatu waliokuja na pikipiki (bodaboda) na kuanza kuzungumza naye kama
marafiki kwa takribani saa nzima na baadae binti yake kuaga akitaka
kuwasindikiza na hakurudi tena.
Aidha Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Madale, Gration Mbelwa
ameliomba Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kuwaomba
wanafamilia pamoja na rafiki za binti huyo kutoa ushirikiano kwa Jeshi
la Polisi ili kuwakamata watuhumiwa hao.
chanzo:zanzibar24.
Comments