Kutokana na hayo, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amemjibu kwa kusema serikali haipati kigugumizi chochote juu ya jambo hilo kwa kuwa ni la hiyari na wala siyo lazima.
“Kwanza kiujumla ni lazima ieleweke dhana ya ridhaa kwenye huduma za afya na tiba kwa sababu ni jambo la hiyari kama vile ilivyo kwa matibabu mengine yote ni lazima mtu atoe ridhaa yake ndipo aweze kupatiwa huduma ya kufanyiwa tohara na haiwezi hata siku moja kuwa ni jambo la lazima. Na kwa msingi huo serikali haina kigugumizi chochote juu ya hilo”, amesema Dkt. Kigwangalla.
Kwa upande mwingine, Dkt. Kigwangalla amesema tohara inapunguza maambukizo ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)kwa asilimia 60 hivyo amewataka wanaume wote ambao bado hawajafanyiwa tohara kutumia nafasi hiyo kwenda kwenye vituo vya kutoa huduma hiyo ili waweze kupewa huduma hiyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments