Kampuni
ya udalali ya YONO imesimamia shuguli za kuuzwa kwa mnada gorofa
lililopo upanga mali ya kampuni ya Lugumi Enterprises Limited na
kununuliwa na kampuni ya Al-Naeen Enterprises kwa shilingi Milioni 700.
Mnada
huo wa magorofa hayo na majengo mengine mawili ambayo yamekosa wateja
kutokana na bei zake kuwa juu ukilinganisha na ukubwa wa jengo bado
hayajapatiwa wateja.
Akizungumza
wakati wa mnada huo, Mkurugenzi wa kampuni ya YONO Scolastica Kevela
amesema kuwa Nyumba ambazo zimekosa wateja zinauzwa Shilingi Milioni 460
na zinapatikana eneo la Mbweni JKT Wilaya ya Kinondondi jijini Dar es
Salaam.
Kampuni
ya Lugumi Enterprises Limited inahusishwa na kashfa ya ubadhirifu wa
fedha za serikali pamoja na kudaiwa kodi na TRA masuala ambayo
yamepelekea kuuzwa kwa majengo hayo na kulipia kodi TRA.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments