Katibu
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Vincent
Mashinji amehojiwa na polisi kuelezea namna anavyowafahamu watu
waliofanya shambulio la risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu.
Akizungumza
jana baada ya kutoka katika mahojiano hayo na maofisa wa polisi, Dk.
Mashinji alisema maofisa hao walimtaka kuelezea alichowaambia waandishi
wa habari katika mkutano wake nao mara baada ya kutokea kwa tukio hilo
ambapo alionyesha dalili ya kuwafahamu waliohusika na tukio hilo.
“Niliwataka kurejea kwenye yale mazungumzo ili kuangalia kama nilionyesha dalili ya kuwafahamu watu hao au la.
“Baada
ya kuwaambia hivyo walirejea kwenye mazungumzo hayo na kubaini kuwa
katika kauli zangu sikuonyesha kama nilikuwa nawajua watu hao bali
niliwataka wananchi kufufua polisi jamii ambayo itasaidia kuimarisha
ulinzi,” amesema.
Dk.
Mashinji amesema kutokana na hali hiyo, maofisa hao wa polisi walitaka
kujua kama anazo taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo ambapo alijibu
hana taarifa hizo ila aliwataka polisi kuhakikisha waliofanya tukio hilo
wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria.
Mahojiano
hayo ya polisi na Dk. Mashinji, yanatokana na wito wa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ambaye alimtaka kiongozi huyo kufika
kwenye Ofisi ya Polisi ya Mkoa wa Dodoma au Ofisi ya DCI kwa ajili ya
mahojiano.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments