Hospitali ya Mount Meru ambayo imehifadhi mwili wa kijana Samson Peter aliyekuwa akiteka na kuwaua watoto wawili imesema bado hawajapokea taarifa zozote kuthibitisha taarifa wanazozisikia kwenye vyombo vya habari kuwa familia ya marehemu imegoma kuzika mwili huo na kwamba hadi sasa mwili huo bado wameuhifadhi hospitalini hapo.
Msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitalini hapo, Francis Coster amesema kupitia televisheni kuwa hakuna ndugu wala jamaa wa karibu yeyote aliyejitokeza kuja kudai mwili kwaajili ya maziko na taratibu za maziko ya marehemu ambao ndugu zao hawakujitokeza mapema hospitali kuwachukuwa wao huwafanyia taratibu za mazishi baada ya siku 21.
Samsoni alifikwa na mauti kwa kupigwa risasi na Polisi Murieti Jijini Arusha September 6, mwaka huu alipojaribu kutoroka mikononi mwa polisi wakati akienda kuwaonesha askari hao watu alioshirikiana nao kufanya utekaji na mauaji ya watoto wawili.
chanzo:zanzibar24.
Comments