Daktari
Mfawidhi wa Gereza la Keko, Inspekta Eliud Mwakawanga ameileza Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi maisha ya mfanyabiashara Yusufu Manji
yalivyokuwa gerezani kwamba alikuwa akitumia vidonge kati ya 25 mpaka 30
kwa siku.
Ameeleza
kuwa walikuwa wakipatia dawa hizo alipokuwa akisikia aumivu hasa ya
mgongo na kwamba kuna kipindi alikuwa anaamka akiwa na hali ya
kutetemeka au kuchanganyikiwa.
Pia
ameeleza kuna wakati Manji alikuwa anaamka anashindwa hata kutembea na
wakati mwingine alikuwa akitumia mkanda kufunga mgongo.
Shahidi
huyo wa sita wa upande wa mashtaka ametoa ushahidi huo leo Jumanne
katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili
Manji.
Ameeleza
kuwa Julai 6, 2017 walimpokea Manji akitokea Hospitali ya Muhimbili
Kitengo cha Moyo cha JKCI ambapo waliambiwa ni mshtakiwa lakini ni
mgonjwa.
“Nilienda kumuona, tukazungumza naye na tulikaa naye gerezani hadi alipokuja kuachiwa,”
"Tangu
nimempokea hali yake kiafya haikuwa nzuri na alikuwa mtu anayetumia
dawa wakati wote na alikuja na dawa zake za aina sita kutoka Muhimbili
ambazo alikuwa akizitumia, pia kulingana na hali yake na mazingira
anayokuwa anajisikia, tulikuwa tukimpatia dawa gerezani mbali na hizo."
Ameeleza
kuwa utaratibu wa kuwapatia dawa mahabusu na wafungwa huwa wanakaa nazo
wao wataalam na wanawapa kutokana na maelezo ya daktari yaliyopo kwenye
cheti ambapo Manji kuna dawa alikuwa anakunywa asubuhi na jioni na
nyingine kulingana na hali yake ya siku hiyo.
Shahidi huyo ameeleza kuwa wao huwa hawatoi dawa za kulevya kwa mgonjwa ila wanatoa dawa.
Alisema hivyo baada ya kuulizwa na Wakili Hajra Mungula kuwa dawa walizompatia Manji zinahusiana vipi na dawa za kulevya.
"Sijachunguza
sana kuona zina uhusiano gani na dawa za kulevya,” ameeleza na
kusisitiza wao hawatoi dawa za kulevya kwa mgonjwa wanatoa dawa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments