
Akitoa taarifa juu ya utekelezaji wa maagizo ya kamati ya kudumu ya
baraza la wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa
kwa mwaka wa fedha 2017 hadi 2018 Waziri wanchi Ofisi ya Makamo wa Pili
wa Rais Mohammed Aboud Mohammed amesema ongezeko hilo ni la asilimia 36
ulikinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha 2016 hadi 2017 ambapo zaidi
ya shiling milioni mianne na salasini na sita zilitolewa kwa ajili ya
shughuli hizo zimelenga kupambana na janga hilo.
Amesema kuwa serikali imeamua kuongeza bajeti hiyo ili kufikia lengo
la kudhibiti uingizwaji na usafirishaji wa dawa za kulevya nchini
pamoja na kukabiliana na matatizo yanayojitokeza katika uendeshaji wa
kazi hizo.
Kwaupande wao baadhi ya Wajumbe Akiwemo Soud Said Soud na Riziki
Pembe Juma Wakizungumza na Zanzibar24 mara baada ya kuwasilisha kwa
Ripoti hiyo wametoa maoni yao juu ya kutafuta mikakati imara ya
kukomesha uingizaji na ushambazaji wa madawa ya kulevya nchini.
Wamesema endapo sheria zilizopo zitatumika bila ya muhali
itasaidia kwa kiasi kikubwa kupamba na kuwakamata wahalifu wa madawa
ya kulevya nchini.
Aidha wametoa wito katika jamii kutoa ushirikiano kwa serikali
katika kuwafichua wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya kwani
serikali imejipanga kuwatia nguvuni na kuwafikisha katika vyombo vya
sheria.
chanzo:
Comments