
Rick Scott , asema kwamba vipaumbele vya haraka
vimeelekezwa katika kusaidia hospitali na kuokoa maisha. Zaidi ya
theluthi mbili ya taifa hilo haina nishati ya umeme na bwana Scott
amearifu kuwa itachukua wiki kadhaa kurejeshwa kwa ukamilifu wake
nishati hiyo.
Moja ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga
hicho ni maeneo ya pwani ya mji wa Florida yajulikanayo kama vitovu vya
Florida na imearifiwa kuwa itachukua muda kwa wakaazi wa maeneo hayo
kurejea katika makaazi yao.
Scott anasema Kuna uharibifu mkubwa , nina matumaini kila mtu alinusurika, ni mambo ya kutisha tuliyoyaona.
Ninajua
hali ya taifa letu lakini hasa vitovu vya Florida itachukua muda
kurejea katika hali yake ya kawaida, kwakweli kuna uharibifu mkubwa .
''Naelewa
kuwa watu walio wengi wanataka kurejea katika maisha yao ya kawaida,
najua kila mmoja anataka kuanza upya, nawasihi kuwa na subra, mnapaswa
kupata msaada wa haraka katika maeneo yenu, tunapaswa kupata maji tena,
tunahitaji huduma zote za kijamii zirejee kama kawaida lakini nasema,
itachukua muda nrefu!''
chanzo:Bbc.
Comments