
Taarifa hiyo imetolewa leo na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini ACP
Barnabas David kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, na kuwataka
watu hao akiwemo mbunge huyo wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA kujisalimisha
wenyewe kwa kutoa taarifa za uongo.
ACP David ameendelea kwa kusema kwamba jeshi la polisi kitengo cha
upelelezi wa makosa ya mtandaoni kinaendelea na uchunguzi, kuwabaini
wote waliohusika na kusambaza kwa taarifa hizo za uongo ili hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yao.
chanzo: zanzibar24.
Comments