Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema kuwa mjumbe wa kamati kuu
ya chama hicho Tundu Lissu anaendelea vizuri na ameshazinduka.
Akizungumza
na vyombo vya habari leo Ijumaa, Dk Mashinji amesema amezungumza na
mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambaye aliongozana na Lissu
kupata matibabu Nairobi nchini Kenya na amemueleza kuwa Lissu anaendelea
vema na amezinduka baada ya dawa alizochomwa kwa ajili ya kupumzika na
kusafiri kuisha.
Amesema
damu ya Lissu imemwagika kabla ya wakati wake hivyo makamanda wa chama
hicho nchi nzima waende kwenye hospitali na zahanati kutoa damu.
"Tuchangie damu kuhakikisha benki za damu zinakuwa na damu ya kutosha ili ziwasaidue wahitaji," amesema Dk Mashinji.
Dk Mashinji amesema tukio hilo halijawatisha badala yake limewaimarisha zaidi.
Alifafanua kuwa Lissu alimiminiwa risasi za kutosha kuashiria kulikuwa na lengo la kuua.
Kwa
upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Profess Abdallah Safari
amesema wao kama wanasheria likitokea jambo kama lililomtokea Lissu
huangalia mambo mawili makubwa, ambayo ni imetumika silaha gani na
amepigwa eneo gani, hivyo kwa Lissu alilengwa kupigwa kichwa na kifua
kuonyesha wazi kulikuwa na nia ya kuua.
"Hali inatia simanzi watu wa usalama wafanye kazi yao kwa weledi kulibainisha hili,"alisema Profesa Safari.
Waziri
mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema kazi kubwa ya Serikali ni
kulinda usalama wa raia, kama imeshindwa kufanya hivyo inaonekana wazi
kuna kasoro za uwajibikaji.
"Kwa
sisi tuliofanya shughuli za uongozi siku nyingi uwajibikaji unaweza
kukosekana kwa makusudi au kwa uwezo na kupanga," amesema Sumaye.
chanzoa;Mpekuziblog.
Comments