Makamu
Mwenyekiti wa CHADEMA Bara na Wakili wa kujitegemea Tanzania. Prof
Abadallah Safari amesema wao kama CHADEMA hawana imani na uchunguzi
utakaofanywa na jeshi la polisi au serikali kuhusu shambulio la kujaribu
kumuua Mbunge Tundu Lissu.
Akizungumza
na wanahabari wakati wakitoa taarifa ya kamati kuu kupitia kikao
walichokaa mwishoni mwa wiki iliyopita, Prof. Safari amesema kuwa wao
hawana nia mbaya ya kutaka uchunguzi kufanywa na wachunguzi wa mambo ya
nje lakini hii ni kutokana jinsi tukio lilivyotokea.
"Hatuna
nia mbaya lakini sisi kama CHADEMA hatuna imani na serikali pamoja na
jeshi lake la polisi katika uchunguzi wa jaribio la mauaji ya Mbunge
wetu. " alisema Prof Safari.
Pamoja
na hayo Prof. Safari amedai anamshangaa sana Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini , IGP Simon Sirro, kwa kauli yake ya kwamba Tundu Lissu hakufika
kuripoti tukio la kufuatiliwa na watu asiowajua na kusema kuwa huko ni
kutojua sheria ya mmwenendo wa makosa ya jinai.
Amesema
kuwa Sheria hiyo inaeleeza namna jeshi lapolisi linavyotakiwa kufanya
kazi zake na kwamba jeshi la polisi kazi yake ni kufuatilia na kufanya
upelelezi juu ya taarifa kwani wao ni walinzi wa amani na kuongeza
kwamba Lissu tayari alieleza kila kitu lakini polisi hawakujali.
"Hatuamini
kama walikuwa hawajui kama kuna taarifa Lissu alizitoa kuhusu yeye
kufuatiliwa au waliamua tuu kutotilia maanani" alisisitiza Prof.
Safari.
Mbali
na hayo Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vicent Mashinji ameeleza kwamba
kwa sasa wanachohakikisha ni kwamba hospitali aliyopo Lissu inazidi
kuimarishwa ulinzi lakini pia hatoweza kuzungumzia hali yake kwa undani
kutokana pia na kuwepo watu wasiokuwa na nia njema.
chanzo:mpekuziblog.
Comments