Ashambuliwa kwa kupigwa mawe, mapanga na marungu huko Fuoni Melitano.

Kijana mmoja mshirazi wa Mwanakwerekwe ameshambuliwa na  watu wasiojulikana kwa kupigwa marungu, mawe na mapanga huko Fuoni Melitano, wilaya ya Magharibi B Unguja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi Unguja Hassan Nassir Ali amesema watu wasiojulikana  walimshambulia kijana Said Moh’d  Said miaka 26 na kumsababishia majeraha katika sehemu mbali mbali za mwili wake.

Kamanda amebainisha kuwa majeruhi yupo katika hospitali ya mnazi mmoja akiendelea kupata matibabu.
Aidha amesema jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kuwabaini wahalifu na kubaini chanzo cha tukio hilo ambalo lilifanyika tarehe 7,9 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana  huko Fuoni  Melitano.
chanzo:zanzibar24.

Comments