Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na mwenzake kulipa faini
ya Sh35 milioni kila mmoja au kutumikia kifungo cha miaka sita jela.
Mbali na Mattaka, mshtakiwa mwingine ni Elisafi Mathew aliyekuwa kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha cha ATCL.
Uamuzi huo umetolewa na Mahakama baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.
Akitoa
hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa alimuachia huru
William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL, baada ya
upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka
dhidi yake.
Mahakama
pia imeamuru Mattaka na Mathew kulipa hasara waliyoisababishia ATCL
katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni Dola 143,442.75 za
Marekani ndani ya mwezi mmoja.
Washtakiwa
walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabili ya kula
njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Serikali
chanzo:Mpekuziblog.
Comments