Ajinyonga baada ya kumnajisi ng’ombe Pemba.

ajinyonga
Kijana mmoja mkaazi wa Ole kipangani ame jinyonga kwa kutumia shuka ndani ya chumba chake, muda mfupi baada ya kuonekana akinajisi ng’ombe.

Kijana huyo alie tambulika kwa jina la Hamad Omar Juma mwenye umri wa miaka 17 Inaaminika kwamba  alijinyonga baada ya kupatwa na fazaa kwenye akili yake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Sheikhan Mohammed Sheikhan, alisema tukio hill lilitokea Septemba 25 saa 6.30 mchana.
Alisema awali marehemu alimnajisi ng’ombe katika eneo la kipangani na baada ya kuenea taarifa hizo kwa wananchi, alipatwa na fazaa kubwa katika akili yake na ndipo alipoamua kujinyonga.
Alsiema mwili wa marehemu ulipelekwa hospitali ya Chake Chake na baadae kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.
Alisema bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Aliwataka wazazi kuwa karibu na vijana wao na kuwasikiliza ili kama wana matatizo waweze kuyafanyia kazi ikiwemo kuwapa ushauri.
chanzo:zanzibar24.

Comments