22 wafariki katika mkanyagano kwenye reli India.

Watu kumi na mbili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia kisa cha mkanyagano baada ya daraja moja kuporomoka karibu na kituo cha treni, mjini Mumbai India.
Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahala hapo kujikinga.

Watu waliojeruhiwa wamefikishwa katika hospitali iliyo karibu na maafisa wakuu wa reli wapo katika eneo la mkasa.
Msemaji wa shirika la reli Anil Saxena ameambia waandishi habari kuwa daraja hilo lililofunikwa lilikuwana shughuli nyingi kwasababu idadi kubwa ya wasafiri waliokuwa wanajikinga na mvua kubwa walijaribu kuondoka kwa wakatimmoja na abiria wengine.
Ameongeza kuwa mkasa huo utachunguzwa.
chanzo:zanzibar24.

Comments